Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*MBRAZIL ANDREY COUTINHO AKABIDHIWA JEZI YA DIDIER KAVUMBAGU YANGA

$
0
0
Na Sufianimafoto Reporter, Dar
KIUNGO mpya wa Yanga Mbrazil, Andrey Coutinho, amewataka mashabiki wa Klabu hiyo na wanachama kuondoa hofu na kusubiri kupata raha na burudani ya soka kutoka kwa Klabu yao, iliyoanza mazoezi ya kujiandaa na Ligi kuu Bara msimu wa 2014-2015 na ile ya Shirikisho.
Kiungo huyo aliyekabidhiwa Jezi namba 7, iliyokuwa ikivaliwa na Mshambuliaji Mburundi, Didier Kavumbagu aliyetimkia Azam Fc, amesaini mkataba wa miwaka miwiki kuitumikia Klabu hiyo.
Mbali na Kiungo huyo, pia Uongozi wa Yanga umemtuma mmoja kati ya viongozi wake kukwea Pipa kuelekea Brazil kwa ajili ya kunasa wachezaji kadhaa alioelekezwa na kocha mpya wa Yanga, Marcio Maximo, ili mmoja kati yao aweze kutua Bongo kujiunga na Klabu hiyo.
Maximo amewapa Yanga SC mawasiliano ya wachezaji kadhaa wa Kibrazil wanaocheza nchini humo, ili waweze kuonana na viongozi wa Yanga wakitua nchini humo na iwapo wakiridhishwa na viwango vyao waweze kufanya mchakato wa kutua nao nchini.
Ujio wa Kiuongo huyo na iwapo atatua Mbrazil mwingine katika kikosi hicho, Yanga SC itakuwa ikitimiza mpango wake wa kuachana na Mganda mmoja wapo kati ya Hamisi Kiiza au Emmanuel Okwi, kwa kuwa idadi ya wachezaji wa kigeni katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwisho ni watano tu.
Wachezaji wageni waliokwisha saini mkataba Yanga ni  beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima kutoka Rwanda, Coutinho wa Brazil, Kiiza na Emmanuel Okwi wote wa Uganda- maana yake ili kuongeza mchezaji mwingine wa kigeni itatakiwa kupunguza mmoja, ambapo  na Diego wa Kampala yuko kwenye mstari mwekundu.
Yanga SC imekwishaanza mazoezi rasmi chini ya makocha wake wapya, Wabrazil Marcio Maximo na Msaidizi wake, Leonardo Neiva, asubuhi ikijifua katika fukwe za Coco na jioni Uwanja wa Chuo cha Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam.
Yanga SC inatarajia kushiriki Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame mwezi ujao mjini Kigali, Rwanda na ikirudi itafungua pazia la msimu wa Ligi Kuu kwa kumenyana na mabingwa Azam FC katika mechi ya Ngao ya Jamii mwezi huo huo.
Na baadaye mapema mwakani, Yanga SC iliyomaliza nafasi ya pili msimu uliopita katika Ligi Kuu, itashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>