Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*LIGI YA WANAWAKE MKOA WA DAR ES SALAAM KUANZA AGOSTI 28

$
0
0
LIGI ya Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam inatarajiwa kaunza Agosti 28 mwaka huu katika viwanja vya  Benjamin Mkapa, Bandari na Makurumla.

Ofisa Habari wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Mohamed Mharizo alisema kuwa ligi hiyo ni moja ya mkakati wao wa kuimarisha mchezo ili uweze kuwa na hamasa kwa wanawake.

Alizitaja timu zitakazoshiriki ligi hiyo kuwa ni Mburahati Queens, Evergreen Queens, Sayari, Real Tanzanite, Uzuri Queens,  Simba Queens,  BYC Queens, JKT Queens,  Lulu Queens,  Mchangani Sisters, TMK Queens, Msimamo Queens na Mikocheni Queens.

“Kwa kweli ligi ya wanawake nayo ni muhimu kama ilivyo kwa wanaume, lengo letu ni kuona wanawake wanakuwa na ligi yao na sisi tunaona hili ni jambo zuri ambalo litasaidia kupata wachezaji wa timu ya taifa (Twiga Stars).

Mharizo aliyaomba makampuni na taasisi mbalimbali kujitokeza kudhamini ligi hiyo ili iweze kuleta ushindani kwa timu shiriki.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>