Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akizungumza na baadhi viongozi na wajumbe kutoka Chama cha Wakulima Wadodowadogo wa zao la Pamba Tanzania(TACOGA) katika ukumbi wa mikutano wa Bunge wa Pius Msekwa leo wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma kwa lengo la kuwasilisha Azimio la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa mahitaji ya wakulima Tanzania.
Kaimu Mwenyekiti wa kutoka Chama cha Wakulima Wadodowadogo wa zao la Pamba Tanzania(TACOGA), Godfrey Mokiri(katikati) akizungumza na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta(kulia) katika ukumbi wa mikutano wa Bunge wa Pius Msekwa leo wakati baadhi viongozi na wajumbe wa chama hicho walipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma kwa lengo la kuwasilisha Azimio la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa ardhi kwa mahitaji ya wakulima Tanzania.Kushoto ni Katibu wa chama hicho, George Mpanduji.
Baadhi viongozi na wajumbe wa Chama cha Wakulima Wadodowadogo wa zao la Pamba Tanzania(TACOGA) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta (wanne kushoto) na Katibu wa Bunge hilo, Yahaya Khamis Hamad (wa tatu kulia )walipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma leo kwa lengo la kuwasilisha Azimio la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa mahitaji ya wakulima Tanzania. Picha na Kamati ya Bunge Maalum la Katiba
********************************
********************************
Na Magreth Kinabo, DODOMA
Chama cha Wakulima Wadodowadogo wa zao la Pamba Tanzania(TACOGA) kimemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe . Dkt . Jakaya Mrisho Kikwete asisitishe mchakato wa mijadala ya Bunge Maalum la Katiba , kwani kitendo cha kusitisha ni kuzuia makusanyo ya mawazo mtambuka ya wabunge .
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu chama hicho, George Mpanduji wakati akizungumza na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta Maalum ofisini kwake mjini Dodoma leo kwa lengo la kuwasilisha Azimio la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa mahitaji ya wakulima Tanzania.
Mpanduji aliambatana na baadhi wa viongozi na wajumbe kutoka mikoa 11 wa TACOGA ,alisema wanaheshimu makubaliano ya kisiasa ya kutungwa Katiba ya Nchi, lakini tunatahadharisha kuwa shurti za kisiasa zinazopiganiwa na vyama vya upinzani Bungeni hadi kuzuia wabunge kutetea haki mtambuka za kijamii suala hilo linaleta hitilafu ya kuchelewesha mahitaji muhimu kama ya kujengwa amani kati ya wakulima na wafugaji.
“ Vikao vya Bunge Maalum viendelee na wabunge wote watangulize kwanza maslahi ya umma dhidi ya misukumo batili iliyo kinyume na maslahi mapana ya umma na taifa. Wabunge hawa wanafikra chanya za kujenga makutano ya fikra patanifu ya kupatikana suluhu za haki za makundi mbalimbali, hususani pale palipo na ombwe la matakwa hayo Katika ya sasa,” alisema Mokiri.
Aidha Mpanduji aliongeza kwamba wanashauri agenda za haki mbalimbali kwa jamii zipewe vipaumbele kwa kuwa pana vilio vya kuhitajika suluhu za haraka kwa mahitaji mbalimbali ya makundi ya umma.
Mpanduji alisema wakulima hao, wanataka Katiba ipatiokane haraka kwani itakuwa suluhisho dhidi ya mizozo na maafa yanayotokea nchni kati ya wakulima na wafugaji.
“ Tunahimiza vyama vya siasa vishindanishe hoja za kukonga mioyo kwa kutetea haki za jamii na taifa dhidi ya kutambulisha misukumo y shurti za utashi wa makundi ya watu ya maslahi binafsi,” alisisitiza.
Alisema chama hicho ,pia kinampongeza Mhe. Sitta kwa uvumilivu wake na hekima ya uongozi na wabunge wote wanaohudhuria vikao vya Bunge hilo kwa kuwa wanatimiza uzalendo wao, uaminifu wao na utiifu wao wa kutumikia jamii na taifa.
Chama hicho kimtaka mlezi wao ambaye ni John Shibuda Mbunge wa Jimbo la Maswa Maghribi, ambaye waliochagua kuanzia mwaka 2012 kuendelea kuhudhuria vikao vyote vya Bunge hilo ili akasimamie maslahi yao na aungane na vikundi vinavyoandaa na kutetea haki za wakulima Tanzania.
Kwa upande wake Mhe. Sitta alisema lengo la kutungahiyo ni iwe rafiki yenye kukidhi matakwa ya wananchi.
Miongoni mwa hoja nyingine walizozungumzia ili Katiba itamke ni haki ya mikopo kwa wakulima, ruzuku wa wakulima, iwalinde na itamke haki za wanawake katika kumiliki ardhi wanapofiwa na waume zao na kufadika na mapato ya kilimo.