Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*MADUKA YA KARIAKOO BADO NI MGOMO MENGINE NI KAMA KAWAIDA, VURUGU KUBWA YAZUKA KATI YA WALIOFUNGUA NA WALIOFUNGA

$
0
0
 Katika Mtaa huu unaotoka Sokoni Kariakoo kupanda hadi Mtaa wa Mchikichi hivi ndivyo unavyoonekana siku ya leo asubuhi majira ya saa nne ukiwa kimya hauna msongamano wa watu na magari kama ulivyozoeleka siku maduka yote ya eneo hilo yakiwa wazi, ambapo unakuwa msongamano mkubwa wa watu na magari. Habari zilizoufikia mtandao hivi sasa zinasema kuwa vurugu kubwa imezuka mitaa hiyo ya Kariakoo baina ya wafanyabiashara wenyewe kwa wenyewe kati ya waliofungua maduka na wale waliofunga maduka huku waliofunga waliwashinikiza waliofungua nao kufunga maduka yao ili kuendeleza mgomo huo.
 Baadhi ya wafanyakabiashara wa maeneo hayo wakiwa wamepumzika huku wakipiga stori nje ya maduka yaho wakiwa hawana hata mpango wa kufungua maduka hayo kufuatia mgomo wao kuhusu mashine za EFD's uliofikia siku ya nne sasa. 
  Baadhi ya wafanyakabiashara wa maeneo hayo wakiwa wamepumzika huku wakipiga stori nje ya maduka yaho wakiwa hawana hata mpango wa kufungua maduka hayo kufuatia mgomo wao kuhusu mashine za EFD's uliofikia siku ya nne sasa. 
 Wengine wakiendelea kununua bidhaa kama kawaida....
 Wengine walikuwa wakisikitika kama hivi...
 Wengine wakipiga stori tu...
 Baadhi ya maduka yalikuwa wazi yakiendelea kutoa huduma kama hivi wanavyoonekana pichani..
 Huyu pia ni mfanyabiashara akitoka kununua bidhaa katika baadhi ya maduka yaliyowazi.
 Hapa wafanyabiashara wakiendelea kupata huduma....
 Hapa hakuna mgomo ni kama kawaida tuuuu......
 Hawa ni baadhi ya wafanyakazi wa katika maduka haya yaliyofungwa wakiwa hawajui la kufanya wakati mabosi wao walipoamua kufunga maduka.
 Hawa nao wakipiga stori tu hadi muda ufike wakurudi nyumbani....
 Maduka yakiwa yamefungwa....
Maduka kibao yakiwa yamefungwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>