Mfanyabiashara wa Kuku (katikati) akiwa katika mitaa ya Kariakoo, akisubiri wateja wa kuku. Katika kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu ya Iddi, baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga wamekuwa wabunfu kuendana na alama za nyakati na matukio yanayojitokeza na sio kutegemea biashara ya aina moja wakati wote, ambapo hivi sasa wengi wao wamehamia katika biashara kama hizi ambazo wameona kuwa zinatoka kwa haraka kutokana na Sikukuu iliyo mbele yao. Lakini pamoja na ubunifu huo wamachinga hao wamekuwa wakiuza kila Kuku mmoja Sh. 25, 000/= hadi 20,000/= kulingana na ukubwa wa kuku.
Bei ya viungo nayo imepanda kama bidhaa nyinginezo katika soko la kariakoo.
Katika mtaa huu kila mmoja akiwa katika harakati za kusaka mahela na wengine kusaka mahitaji. Picha zote na Miraji Msala wa Sufianimafoto