Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi kitabu maalum cha kuhamasisha ulishaji bora wa watoto katika jamii wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo mchana. Kushoto ni Waziri wa Afya Dkt. Hussein Mwinyi.
Mama Salma kikwete, akionyesha kitabu hicho baada ya kuzinduaa rasmi. Kushoto ni Waziri wa Afya, Dkt. Hussein Mwinyi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia waalikwa na wananchi wa Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani.yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Baadhi ya wanawake waliohudhuria sherehe za kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani yaliyofanyika Mnazi Mmoja na kufungwa rasmi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahi alipokutana na mtoto Muktar Abdul mwenye umri wa miezi sita akiwa na mama yake Lucia Lingwanda, mkazi wa Chanika, wilayani Ilala, wakati Mama Salma alipotembelea mabanda ya maonesho ya wiki ya unyonyeshaji duniani katika sherehe zilizofanyika Mnazi Mmoja.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwte akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wageni waalikwa kwenye siku ya kilele ya maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja. PICHA NA JOHN LUKUWI