Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*WAZUNGU Katie Gee (18) NA Kristie Trup (18) WAPOKELEWA UINGEREZA CHINI YA ULINZI MKALI

$
0
0
Raia wa Kigeni 'Wazungu' Katie Gee (18) na Kristie Trup (18), wamewasili nchini Uingereza na kupokelewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki huku wakiwa chini ya ulinzi mkali.

Walimu hao wawili wa kujitolea, raia wa Uingereza, walijeruhiwa kwa kumwagiwa tindikali, katika maeneo ya Mji Mkongwe, Shangani, Zanzibar, hivi majuzi.

Madada hao, walivamiwa na kujeruhiwa majira ya saa moja usiku, wakati wakienda kupata chakula cha jioni.

Aidha habari za chini ya Kapeti zinasema kuwa mmoja wa walimu hao alishawahi kushambuliwa wakati akiwa kisiwani humo wiki mbili zilizopita.

Kwa mujibu wa mmoja wa marafiki zao, Oli Cohen, mwenye miaka 21, alisema: "Katie alishambuliwa wiki mbili zilizopita na mwanamke mmoja wa Kiislamu baada ya kumsikia akiimba wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

"Alishitushwa mno na tukio hilo - lakini hakupatwa na hofu kiasi cha kufikiria kurejea nyumbani. Akaendelea kuishi visiwani hapo hadi atakapomaliza safari yake na kazi yake ya kujitolea."
 Katie Gee (18) na Kristie Trup (18)
Katie Gee (18) kabla na baada ya kumwagiwa Tindikali.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>