Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva (wa pili kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Azam Fc, Himid Mao, wakati wa mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii, uliochezwa kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, leo jioni. Katika mchezo huo Yanga ilishinda bao 1-0, bao pekee katika mchezo huo lililofungwa na Salum Telela, katika dakika ya 2 ya mchezo lililodumu hadi mwisho wa mchezo huo.
************************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
BAO pekee la kiungo Salum Abdul Telela, lililofungwa katika dakika ya pili katika mchezo wa leo wa kuwania Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Yanga na Azam Fc, limeiwezesha Yanga SC kutwaa Ngao hiyo na kuendeleza uteja kwa timu hiyo.
Mchezo huo wa leo ulichezeshwa na mwamuzi Oden Mbaga, aliyesaidiwa na Hamisi Chang’walu na Omar Kambangwa wote wa Dar es Salaam.
Hadi timu hizo zinakwenda mapumzika Yanga SC walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0, lililodumu hadi mwisho wa mchezo.
Bao hilo ilikuwa ni pasi nzuri kutoka kwa Didier Kavumbagu iliyounganishwa na Salum Telela katika dakika hiyo ya pili.
Ilikuwa ni Dakika ya 67 Telela alikijipinda kuunganishia krosi nzuri ya Haruna Niyonzima, iliyokwenda nje. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI
Dakika ya 81 Niyonzima alikaribia kufunga mwenyewe kwa mpira wa adhabu, lakini shuti lake liligonga mwamba wa juu na kudondokea chini kabla ya beki Aggrey Morris, kuondosha katika hatari.
Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’/Deo Munishi ‘Dida’ dk15, Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan/Mbuyu Twite dk15, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Salum Telela, Jerry Tegete/Hussein Javu68, Didier Kavumbangu na Haruna Niyonzima.
Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni/Joackins Atudo dk46, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Himid Mao, Kipre Tchetche, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’/Gaudence Mwaikimba dk74, Kipre Balou/Ibrahim Mwaipopo dk62 na Khamis Mcha.
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima (kulia) akimtoka beki wa Azam Fc, Nazir salum, wakati wa mchezo huo.
Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (kulia) akimtoka mchezaji wa Azam Fc, Michael Balou.
Beki wa Azam Fc, David Mwantika (kulia) akimdhibiti Jerry Tegete, wakati wa mchezo huo.
Nahodha wa Azam Fc, Himid Mao, akiwangoza wenzake kupokea Medali baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro' akiwangoza wenzake kupokea Medadi na kupokea Ngao ya Jamii, baada ya mchezo huo.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro' akipozi na Ngao hiyo baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiki.
Kipa namba moja wa Yanga, Mustafa Bartez, akitolewa nje baada ya kuumia.
Ni pozi la 'Snap' tu, hapa ni Kiungo mkabaji wa Yanga, Athuman Iddi 'Chuji' akipozi na mtangazaji wa Televisheni ya Chanel 5, Patrick Nyembela, wakishow love.......