Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*HII NDIYO NDEGE YA TANZANAIR ILIYOTUA KATIKATI YA ZIWA MANYARA JANA

$
0
0
 Hii ndiyo  Ndege Ndogo ya Shirika binafsi la Ndege la TANZANAIR iliyokuwa ikitokea Mjini Bukoba kuelekea Jijini Dar es Salaam kupitia Zanzibar, ililazimika kutua katikati ya Ziwa Manyara lililopo Mkoani Arusha ili kunusuru abiria wake sita (6) waliokuwamo katika ndege hiyo baada ya kupatwa na hitilafu kwa kuzima ghafla kwa Injini moja wakati ikiwa hewani. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Kamanda Liberatus Sabas, amethibitisha kutokea kwa ajali hilo  jana mchana katika maeneo ya Lambi, kusini mwa wilaya ya Babati. 

 Kamanda Sabas  amesema rubani wa ndege aliyetajwa kwa jina moja la Kondo, ambaye hakudhurika katika ajali hiyo, alitaka kutua ghafla katika viwanja vya  Arusha na Manyara baada ya kutokea hitilafu hiyo, lakini alishindwa baada ya kuona mtikisiko ukizidi na kuamua kuielekeza ndege hiyo katikati ya Ziwa hilo, ambapo alifanikiwa kutua salama.
Baadhi ya Boti na mitumbwi iliyokuwa karibu ilisogea na kutoa msaada wa kubeba abiria hao na kuwasogeza nchi kavu na baadaye ilifika Helikopta ambayo iliweza kutoa msaada zaidi.
Ndege ya Shirika la ndege la Tanzanair ikiwa katikati ya maji ziwa Manyara jana baada ya kupata hitilafu katika injini moja wakati ikiwa hewani na abiria sita waliokuwamo kukimbizwa hospitali ya Siryan mkoani Arusha.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>