Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*SIMBA YATAFUNA MUWA WA MTIBWA SUGAR 2-0

$
0
0
 Kiungo Mshambuliaji wa Simba, Amri Kiemba (kushoto) akiwania mpira na beki wa Mtibwa Sugar, Shaban Nditi, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini dar es Salaam. Katika mchezo huo, Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-0.
************************************
BAO la dakika ya 90+, lililofungwa na Betram Mwombeki, limeiwezesha timu ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, dhidi ya Mtibwa Sugar, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Bao la kwanza la Simba lilifungwa na Henry Joseph, aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Said Hamis, katika dakika ya 67.  
HUKO KWINGINEKO:- COASTAL UNION -0 PRISONS- 0
RUVU SHOOTING -1 MGAMBO SHOOTING- 0
JKT-1 ASHANTI UNITED- 0
YANGA-1 MBEYA CITY-1
AZAM-1 KAGERA SUGAR-1
OLJORO-1 RHINO RANGERS 1
 Mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe (kushoto) akijiandaa kupiga shuti, huku akibanwa na beki wa Mtibwa Sugar, Dickson Mbeikya, wakati wa mchezo huo.
 Beki wa Mtibwa Sugar, Hassan Ramadhan (wa pili kushoto) akitako kuchukua mpira mbele ya beki wa Simba, Issa Rashid, wakati wa mchezo huo.
 Mashabiki wa Simba, wakishangilia bao la pili.
 Mfungaji wa bao la kwanza la Simba, Henry Joseph (kulia) akiwafinya mabeki wa Mtibwa Sugar.
Beki wa Simba Issa Rashid (kulia) akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Ally Shomari.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>