Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*BALOZI IDDI ATEMBELEA KUKAGUA MAJENGO YA SKULI YA SEKONDARI ILIYOTELEKEZWA NA MKANDARASI

$
0
0
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar pamoja na Uongozi wa Wizara ya Elimu Zanzibar akitembelea majengo ya Skuli Mpya ya Sekondari ya Wilaya ya Kusini Iliyopo Paje Mtule ambayo Mkandarasi wake ameingia Mitini kabla ya kukamilisha kazi yake. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Ali Juma Shamhuna akitoa maelezo ya hatua ya ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya ya Kusini iliyopo Baje Mtule mbele ya Balozi Seif aliyefika kukagua majengo ya Skuli hiyo ambayo bado haijakamilika tokea mwaka 2006. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
*********************************
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imeagizwa kumtafuta Mkandarasi mwengine kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa Skuli Mpya ya Sekondari ya Wilaya ya Kusini inayojengwa katika Kijiji cha  Baje Mtule baada ya mkandarasi wa mwanzo aliyepewa jukumu la ujenzi  wa skuli hiyo kukimbia.
Agilo limetolea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi  Seif Ali Iddi alipofanya ziara fupi kuangalia majengo ya Skuli hiyo akiwa pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Ali Juma Shamuhuna pamoja na baadhi ya watendaji wake.
Balozi Seif alisema mkandarasi wa ujenzi wa Skuli hiyo Kampuni ya Electric International Company Limited ya Mjini Dar es salaam alikuwa hana sababu ya kutokamilisha ujenzi huo kwa vile alikuwa akilipwa gharama zake kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba uliopo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba mkandarasi huyo alikuwa na tabia ya kudanganya viongozi Wakuu wa Serikali kwa kutoa sababu zilizopelekea  kuchelewa ukamilishaji wa  kazi aliyopewa kwa visingiio visivyokuwa na msingi.
“ Mimi mwaka jana niliwahi kuja akanidanganya, akaja Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif akamdanganya, hata Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Sheni pia naye akamdanyanga. Sasa tabia hii hatuwezi kuivumilia lazima tutafute Mkandarasi mwengine atumalizie kazi yetu “. Alisisitiza Balozi Seif.

“ Lakushukuru  kwamba kazi kubwa ya ujenzi wa Skuli yetu hivi sasa iko katika hatua za ukamilishaji jambo ambalo limeleta faraja kidogo kwa vile  Serikali haitopata hasara kutokana na mkandarasi huyu kuamua kuingia mitini kabla ya kumaliza kazi yake “. Alifafanua Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Mapema  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamuhuna alisema Shirika la Fedha Duniani { World Bank } limeonyesha nia ya kukubali kugharamia umaliziaji  wa ujenzi  wa Skuli za Sekondari za Wilaya za Zanzibar katika hatua ya awamu ya Pili.

Alisema hatua ya pili imelenga katika ujenzi wa uzio wa skuli hizo ili kuepusha uvamizi wa maeneo ya skuli hizo utakaokwenda sambamba na ujenzi wa Nyumba za Walimu wa Skuli ambapo awali bajeti ya gharama za ujenzi huo ilipungua.

Naye Kamishna wa Elimu Zanzibar Maryam Abdulla alisema kwamba ujenzi huo uliofikia hatua ya kukamilika kwa zaidi ya asilimia 94 hadi sasa umeshagharimu jumla ya shilingi Bilioni 3.4 zilizotolewa na washirika wa maendeleo kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Tarehe 23 machi mwaka 2012 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliiagiza Kampuni ya Electric International Company Limited ya Mjini Dar es salaam kukamilisha ujenzi wa  Skuli hiyo ya Sekondari ya Wilaya ya Kusini iliyopo  Paje Mtule ndani ya kipindi cha miezi minne vyenginevyo itafutiwa mkataba wake.

Msimamizi wa Ujenzi huo alitakiwa kuhakikisha utekelezaji huo unafuatwa mara moja na kinyume chake ni kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ilazimike kuifutia mara moja Mkataba wa ujenzi Kampuni hiyo.

Miezi 15  sawa na mwaka mmoja na miezi mitatu imepita tokea kutolewa kwa agizo hilo la kuifutia mkataba wa ujenzi Kampuni ya Electric International Company Limited ya Mjini Dar es salaam endapo itashindwa kukamilisha ahadi iliyotoa mwezi Machi mwaka 2012.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>