Mshambuliaji wa timu ya Hazina, Seleman Juma (aliyeruka) akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Ras Dodom, wakati wa mchezo wao wa ufunguzi wa mashindano ya SHIMIWI, uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Jamhuri. Katika mchezo huo timu ya Hazina imeibuka na ushindi wa mabao 3-1.
''Napita kushoto, we tulia tu......
Mtanange ukiendelea, ni Beki wa Hazina, Issa Ramadhan (wa nne kulia) akiambaa na mpira wakati wa mchezo huo.
Winga Tereza wa Hazina akichanja mbuga kujiandaa kumimina krosi...

Kipa wa Ras Dodoma, akiokoa moja ya hatari langoni kwake...
Timu zikijipanga kukaguliwa....kabla ya mtanange huo....
Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makala, akisalimiana na wachezaji wa Hazina wakati akikagua timu hizo kabla ya kuanza kwa mtanange huo.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makala, akisalimiana na wachezaji wa Ras Dodoma, wakati akikagua timu hizo kabla ya kuanza kwa mtanange huo.
Katika mchezo wa Netiboli, ilikuwa ni patashika baina ya timu ya Tamisemi na Bunge, ambapo hadi tunakwenda mitamboni Tamisemi walikuwa wakiongoza kwa mabao mengi kwa machache...
Kipute cha netiboli, Tamisemi na Bunge kikiendelea.....
Huyu Centa wa TAMISEMI (mwenye mpira) we acha tu.....
Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia kipute cha netiboli....
Huku nako katika mchezo wa Kamba, ilikuwa ni patashika kati ya timu za wanawake za Hazina na Ikulu, ambapo kwa upande wa wanawake, timu ya Hazina imeweza kuwagalagaza Ikulu, lakini katika picha hizi angalia kama sheria za mchezo huu zinaruhusu triki hii waliyoitumia kina mama hawa ya kukaa chini bila kufanya chochote hadi dakika zilipomalizika na kuibuka na ushindi huo.
Hawa ndiyo Kina Mama wa Ikulu, wakionyesha juhudi zao za sifa ya 'Jiko', lakini haikuwa bahati yao siku ya leo ambapo waliweza kukubali bila kushurutishwa.
Hao bwana kwa kukaa hao weeeeee.........
''Buruza hao wanaanza kukubali wenyewe''......Hapa ilikuwa ni kabla ya kinamama wa Hazina hawaamua kukaa chini, ambapo kamba hii iliganda karibu kwa sekunde nyingi tu....'Chezea Kamba wewe'.....
Huyu ndiye 'Stopa' wa Hazina ambaye alizimika baada ya kuisha kwa dakika za kuvuta kamba ambapo muda wote aligangamala, hapa akipewa huduma ya kwanza........
Kamba kwa upande wa wanaume, Ikulu imeweza kurudisha heshima waliyoporwa Dada zao, ambao na wao waliwaburuza wanaume wa Hazina mara zote mbili na kuibuka na ushindi.
Vuta nikuvute, mwisho wa siku Ikulu (kushoto) waliibuka na ushindi dhidi ya Hazina...