Mabondia Japhet Kaseba (kulia) na Alibaba Ramadhani wa Arusha wakitunishiana misuli wakati wa zoezi la kupima uzito ambapo Kaseba alipata jumla ya Kg 79 na Alibaba Kg 78. Kwa matokeo ya uzito huo mabondia hayo wanaweza kucheza pambano lao bila matatizo na mabondia wanaocheza katika utangulizi wote wapo katika hali nzuri. Pambano hilo litapigwa kesho katika ukumbi wa Friends Corner Manzese kuanzia saa kumi jioni, pambano hilo lililoandaliwa na Ibrahim kamwe wa bigright promotion pia litawakutanisha mabondia zumba kukwe wa kibaha na Jacob maganga wa Tanga,lusekelo daudi na mbaruku heri,issa omar na moro best, mwinyi mzengela na shaban bodykitongoji.harman Richard na Adam yahaya,, shughuli za ndani ya ukumbi na ulinzi zitashughulikiwa na kiwango security na jeshi la polisi hivyo pambano litakuwa katika hali ya usalama zaidi
↧