Gooooo!!!!! bao la sita likifungwa na Hamis Kiiza katika dakika ya 68 baada ya krosi nzuri iliyopigwa na Simon Msuva kutoka winga ya kulia. Katika mchezo huo uliotawaliwa zaidi na Yanga karibu dakika zote za mchezo, Yanga ilianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 1 kupitia mshambuliaji wake, Didier Kavumbagu na bao la pili likipatikana katika dakika ya 2 kupitia winga wake machachari, Simon Msuva.
Mabao mengine yalifungwa na Emmanuel Okwi katika dakika ya 20, Mrisho Ngassa, dakika ya 30, Didier Kavumbagu, dakika ya 53, Hamis Kiiza, dakika ya 68 na la saba likifungwa tena na Simon Msuva katika dakika ya 78.
Kwa ushindi huo sasa Yanga inaongoza msimamo wa Ligi baada ya kufikisha jumla ya Pointi 38, huku Azam Fc, ikirudi nafasi ya pili ikiwa na Pointi, 36 na Mbeya City ikibaki nafasi ya tatu ikiwa na pointi 35 baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Coastal Union kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga, huku mabao hayo yakipatikana katika dakika za 82 na 89.
HUKO KWINGINEKO:- Katika Uwanja wa Manungu mjini Morogoro, Mtibwa Sugar 2 -1 Ashanti United, Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera Sugar 1-0 Rhino Rangers, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Oljoro JKT 1-2 Mgambo Shooting, Uwanja wa Mkwakwani, Coastal Union 2-0 Mbeya City.
Didier Kavumbagu, akibinjuka kupiga Tik Tak mbele ya beki wa Ruvu Shooting, Stephano Mwasika na kipa wake, Abdallah Ramadhan.
Mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi (kushoto) akimchambua kipa wa Ruvu Shooting na kufunga bao la tatu.
Mashabiki wa Yanga, wakishngilia wakiwa na bango linalowakebehi wapinzani....
Simon Msuva (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Ruvu Shooting.
Hatari langoni mwa Ruvu Shooting, Didier Kavumbagu akijaribu kuwania mpira na kipa wa Ruvu.
Wachezaji wa Yanga, wakishangilia bao la sita lililofungwa na Hamis Kiiza.
Hamis Kiiza, akimtoka beki wa Ruvu......
Mabeki wa Ruvu, wakijaribu kumdhibiti Emmanuel Okwi.
Hapiti mtu hapaaaaa, ni Didier Kavumbagu akichuana na beki wa Ruvu....
Said Bahanuzi (kulia) akimtoka beki wa Ruvu.....