Mshambuliaji wa timu ya Taswa Fc, Amani Kinyuki ambaye pia ni mfungaji wa bao la kwanza kati ya matatu, (kushoto) akimfinya beki wa Wahenga Veterans, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa TP Sinza. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare kwa kufungana mabao 3-3 huku Taswa ikitangulia kufunga na kuongoza hadi dakika za majeruhi. Bao la pili lilifungwa na Said Mihogo na la tatu likafungwa na Saleh Ally.
Kiungo mkabaji wa Taswa Fc, Fredy Chuji (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki wa timu ya Wahenga, inayoundwa na wachezaji wa zamani.
Amani Kinyuki (kushoto) akiambaa na mpira akimtoa damu beki wa Wahenga.